Wednesday, February 8, 2012

DULLY AFUNGUKA JUU YA KILI MUSIC AWARDS

mkongwe wa muziki wa bongo flava mwenye hit song kibao Dully Sykes afunguka juu ya kili music awards na kudai hataki kushiriki katika tuzo hizo na hajui kwa ni kwa nini wanamuweka kwenye categolies hizo ikumbukwe yupo katika categories za ''Mtumbuizaji bora,na wimbo bora wa Afro Pop kupitia wimbo wa Bongo flever'' anadai hajaambiwa na alishakataa kuwekwa katika category yoyote katika tuzo hizo kwa sababu tunzo hizo hazimnufaishi kwa lolote ''siitaji na siitaji tuzo yoyote toka tanzania''Dully alisisitiza
hususani kilimanjaro tanzania music award zinazotolewa na kampuni ya kilimanjaro Dully afunguka ''wangejua thamani ya music wangu wangenipa toka kipindi cha hi,bijou,hi,handsome kwa sasa siihitaji tuzo hizo"
lakini habari toka kwa afisa mmoja wa BASATA afunguka juu ya hilo na kudai "wanahitaji uthibitisho wa maandishi toka kwa dully kama awali alivyofanya Mwana FA kupitia gazeti la kita ngoma, basata wanadai hawajapata barua rasmi toka kwa dully"

No comments:

Post a Comment

WEB SEARCH