MGOSI MKOLONI KULIA AKIWA NA SUGU
"NDUGU WAPENDWA.........KUNA TAARIFA MTAIPATA SOON KUPITIA MITANDAO HII YA KIJAMII KUHUSIANA NA SUALA ZIMA LA HARAKATI ZA KUMKOMBOA MSANII WA TANZANIA.............ILA KWA LEO NINGEPENDA KUWAPA TAARIFA IFUATAYO KWA UFUPI TU JUU YA TUNZO HIZI ZINAZOITWA KILI MUSIC AWARD.......
kifupi ni kwamba hakuna msanii yeyote wa Tanzania ambaye atathubutu kusimama hata nchi ya Kenya na kujisifu kuwa ni mshindi wa Tunzo za Kili music award toka Tanzania, kwa sababu hazina heshima yoyote na mbaya zaidi zimejaa fitina,majungu ubinafsi,undugu,ushkaji,kujuana,ufisadi,ukosefu wa taaluma,wizi,upendeleo,unyanyapaa,uwoga na ujinga ndio vimetawala kiasi cha kufanya Tunzo hizi zinakosa heshima na nidhamu kwa sanaa ya muziki Tanzania......silazimishi ukubali ila sijaomba ukatae hapa ninachokimaanisha....JIULIZE.....ni msanii gani wa Tanzania ambaye atathubutu kusema Tunzo zimempatia heshima zaidi ya kupiga picha na kuwekwa kwenye rekodi ambayo wanaharakati watakuja kuifuta soon? nilialikwa kwenye kikao chao cha kwanza pale BASATA na niliwachana live wawape wasanii mkwanja wa kutosha kati ya mil 3 mpaka 5 kwa washindi wakaniona mimi KINEGA ndio maana kwenye kuchagua nominees huko kwenye academy yao Kunduchi wakachaguana wao kwa wao na kuwaacha watu kibao wenye upeo na uelewa wa kutosha kuhusu muziki, japo sikuwa na mpango wa kutaka kuwepo kwa sababu wanajua wasingefanikiwa lazima kingenuka tu,bado nasisitiza suala la heshima ya Tunzo haipo watoe mkwanja kwa wasanii na wote watakaoburudisha wasizingue!!........Nawapongeza wasanii wote waliojitoa kwa kutangaza kwani wako sahihi na ninawaunga mkono...... kitaeleweka........ WASANII TUSIDANGANYIKE!!!
No comments:
Post a Comment